“Upungufu wa Wauguzi Nchini Kenya Wazua Changamoto kwa Huduma za Watoto Wachanga”
Utafiti wa kisayansi uliofanywa na KEMRI-Wellcome Trust kupitia mpango wa Harnessing Innovation in Global Health for Quality Care (HIGH-Q) umeonyesha jinsi changamoto za rasilimali watu zinavyoathiri ubora wa huduma katika vitengo vya watoto wachanga. Utafiti huo umebainisha kuwa upungufu mkubwa wa wauguzi katika hospitali za Kenya ni kikwazo kikuu katika utoaji wa huduma bora kwa watoto wachanga.
Licha ya maendeleo ya kimataifa katika kupunguza vifo vya watoto, vifo vya watoto wachanga bado vipo kwa kiwango cha juu katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Nchi nyingi, ikiwemo Kenya, zinaendelea kujitahidi kufikia lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) la kupunguza vifo vya watoto wachanga. Ingawa kuanzisha teknolojia bora za matibabu katika hospitali kumepewa kipaumbele kama njia ya kuboresha huduma, utafiti unaonyesha kuwa wauguzi ndio nguzo kuu ya mafanikio ya huduma bora kwa watoto wachanga, kwa kuwa wao hutoa huduma ya saa 24 kila siku hospitalini.
Wauguzi ndiyo watoa huduma wakuu kwa watoto wachanga wagonjwa au wale waliozaliwa kabla ya wakati. Majukumu yao ni pamoja na kufuatilia hali ya mtoto, kulisha, kutoa dawa, kuhakikisha usafi na kushughulikia dharura. Hata hivyo, katika mazingira yenye rasilimali chache kama Kenya, upungufu mkubwa wa wauguzi na idadi kubwa ya wagonjwa huathiri vibaya utoaji wa huduma hizi.
Mradi wa HIGH-Q ulifanya tafiti ili kuchunguza athari za upungufu mkubwa wa wafanyakazi katika utoaji wa huduma kwa watoto wagonjwa. Aidha, utafiti ulijikita katika kuangalia athari za kuongezwa kwa wauguzi wa ziada na wasaidizi wa wodi kwa madhumuni ya kusaidia wauguzi katika kazi zisizo za dharura. Pia, mradi huo uliangalia kama mafunzo maalumu juu ya ujuzi wa mawasiliano kwa wauguzi yanaweza kuboresha huduma.
Mradi wa HIGH-Q, unaofadhiliwa na NIHR, ulihusisha hospitali za kaunti nane zilizokuwa sehemu ya Clinical Information Network na ambapo mpango wa Newborn Essential Solutions and Technologies (NEST 360°) ulikuwa umeanzishwa. Kupitia utafiti wa kimaelezo na wa uchunguzi, mradi huu uliangazia maisha ya kila siku ya wauguzi, mazingira ya vitengo vya watoto wachanga, na uzoefu wa akina mama hospitalini.
Matokeo muhimu ya utafiti:
-
Huduma zinazokosekana: Watoto wachanga wagonjwa katika hospitali za umma nchini Kenya hupokea sehemu ndogo tu ya huduma zinazohitajika, jambo linaloonyesha mapengo makubwa katika upatikanaji wa wafanyakazi, mgao wa rasilimali na utoaji huduma. Kwa wastani, wauguzi walikuwa na muda wa kutoa takribani theluthi moja pekee ya huduma zinazotarajiwa, huku baadhi wakihudumia zaidi ya watoto 25 kwa zamu moja.
-
Vikwazo vya muda: Kwa wastani, muuguzi alikuwa na dakika 30 pekee za kumhudumia mtoto mmoja katika zamu ya saa 12—kiwango kilicho chini sana ya viwango vya kimataifa.

Comments
Post a Comment